MKATABA WA MAKUBALIANO BAINA YA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA RELI TANZANIA (TRAWU)

New1

1.0 UTANGULIZI

Mkataba wa Makubaliapo ya pamoja yamefanyika mwezi wa Machi tarehe 10 Mwaka 2011.

Kati ya

Kampuni ya Reli Tanzania, iliyoundwa chini ya Sheria ya Makampuni Na. 12 ya 2002 ya S.L.P. 70364 Mtaa wa Algeria, Dar es Salaam (ambaye ataitwa “Kampuni”) kwa upande mmoja,

Na

Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania, kilichoundwa chini ya Sheria Na. 6 ya mwaka 2004 chenye anwani ya S.L.P. 78458 Mtaa .wa Sofia/Bibi Titi Dar es Salaam (aimbaye ataitwa TRAWU) kwa upande wa pili.

KWA KUWA Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kinaitambua Kampuni ya Reli Tanzania kuwa imewaajiri Wafanyakazi arnbao wengi wao ni wanachama wake.

NA KWA KUWA Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania unakitarnbua Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kuwa ndicho chombo pekee cha Wafanyakazi kinachotetea haki na maslahi yao.

KWA KUWA kila Mamlaka inatambua, kuwepo kwa Mamlaka nyingine Kisheria, na kwamba Wafanyakazi hawa ni kiungc kikubwa cha ushirikiano, 

HIVYO BASI MKATABA HUU UNASHUHUDIA

2.0 WAHUSIKA

Mkataba huu utawahusu Wafanyakazi wote wa Kampuni isipokuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi (Board of Directors) au wale wenye Mkataba maalumu ambao si raia wa nchi hii (Expatriates). Maana ya Wafanyakazi wote kwa rnujibu wa Mkataba huu ni: Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Kampuni.

3.0 UFAFANUZI WA MAAINISHO

Katika Mkataba huu, tafsiri za maneno zimekubalika kama ifuatavyo:-

“Baa”Itakuwa na maana ya mahali ambapo pornbe huuzwa au hunywewa hata kama mahali hapo hapana leseni rasmi ya kileo

“Kanuni”Kanuni ni za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL .Service Regulations)

“Kukaimu Madaraka”Itakuwa na maana ya Mfanyakazi kushikilia madaraka yaliyo juu ya ngazi yake ya ajira.

“Kushikilia nafasi” Itakuwa na maana Mfanyakazi anapokwenda kushikilia nafasi (relieving duties) kwa rnuda usiozidi siku 90 katika kituo kingine.

“Likizo”Itakuwa na maana ya kutokuwepo kazini kwa ruhusa ya Mwajiri

“Likizo ya Ugonjwa”Itakuwa na maana ya kutokuwepo kazini kwa Mfanyakazi kwa sababu za ugonjwa baada ya kupata ushauri wa Daktari aliyesajiliwa na anayetarnbulika na Mwajiri, na kuruhusiwa kiofisi.

“MAC”Itakuwa na maana ya “Management Appointments Committee”

“Mfanyakazi”Itakuwa na maana ya mtu aliyeajiriwa na Kampuni isipokuwa Mkurugerizi Mtendaji, “Expatriates” na wenye ajira za mikataba maalumu.

“Mfanyakazi wa zamu”Itakuwa na maana ya Mfanyakazi aliyepangwa kufanya kazi siku yoyote ya wiki na arnbaye saa zake za kazi si Jazima ziendane na saa za kawaida za Kampuni

“Watumishi Watendaji Katika Treni”

(Running Staff)Itakuwa na maana ya Mfanyakazi yeyote anayefanya kazi katika Tren. Hawa Nipamoja na:

•Dereva wa Treni;

•Dereva wa Treni Msaidizi (Shunter);

•Mhudumu wa Behewa;

•Gadi wa Treni;

•Anayekagua Tiketi ndani ya Treni (Travelling Ticket Examiner, TTE)

•Fundi Umeme (Electrician)

4.0. TAFSIRI YA MKATABA

Mkataba huu ni Mkataba halali baina ya Kampuni na TRAWU na hautengui Sheria zozote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Kanuni na taratibu ndogo ndogo zilizopitishwa chini ya Sheria.

5.0. MADHUMUNI

5.1 Pande hizi mbili zinakubali na kutambua kwarnba:

(a) Ajira ya kuaminika ya Wafanyakazi, maendeleo yao na hali ya maisha yao yanategemea mafanikio, kuwepo na kuendelea kuwepo kwa Kampuni.

(b) Kampuni katika majukumu yake, ina dhamana ya kusafirisha abiria na mizigo. Katika kutekeleza dhamana hiyo, Kampuni, vile vile, ina jukumu la kujiendesha kibiashara.

5.2. Kampuni inatazamia Wafanyakazi wake kuonyesha utii, ari ya kazi na kudumisha kiwango cha juu cha utendaji wa kazi 'kwa-kuzingatia na kuonyesha bidii na nidframu ya kazi. Aid ha, Kampuni inawajibika kwa ustawi na usalama wa Wafanyakazi wake, abiria na mizigo. Hivyo Kampuni na . Chama cha Wafanyakazi wanawajibika kwa pamoja kama ifuatavyo:-

(a) kampuni itawajibika kuandaa miundo ya mishahara na mazingira muafaka ili kuboresha ufanisi wa Kampuni na hali ya ajira kwa Wafanyakazi.

(b) Kampuni na TRAWU watawajibika ktijadili miundo ya mishahara na mazingira ya kazi ili kuepusha migogoro inayoweza kusababisha hasara katika Kampuni.

(c) Kuhamasisha ari ya kazi ili kuleta tija na ufanisi katika mazingira ya amani kazini.

(d) Kudumisha ajira ya uhakika kwa kupambana na aina zote za wizi, uzembe, ulevi, utoro, hujuma na utovu wa nidhamu kazini.

(e) Kusimamia na kuhakikisha usalama na ubora wa nyenzo, vitendea kazi pamoja na mitambo, njia ya reli na majengo ya Kampuni.

(f) Kanuni zozote za ndani ya Kampuni (TRL Service Regulations) zinazopingana na Sheria au Mkataba huu zitakuwa ni batili.

5.3 Kampuni itawajibika kulipa marupurupu yote yaliyomo ndani ya mkataba huu.

MUDA WA MKATABA

6.1 Mkataba huu utadumu kwa kipindi cha miezi ishirini na nne (24) kuanzia tarehe 10 Machi 2011 mpaka 09 Machi, 2013 na utaheshimiwa na utatekelezwa lcipindi chote cha Mkataba. Hata hivyo, Mkataba huu utaanza kutumika rasmi mara tu baada ya kusainiwa, bali tuzo ya kustaafu itaanza tarehe 10 Machi, 2011.

6.2. Wakati wote wa Mkataba huu masharti ya utumishi ya hali bora za kazi yatakuwa kama ilivyo ndani ya Mkataba huu, ila marekebisho na miundo mipya ya mishahara yanaweza kujadiliwa kila baada ya miezi kumi ria mbiii (12) kutegemeana na tija.

AJIRA

7.1. Utaratibu wa kujaza nafasi za kazi

Mara inapotokea nafasi, ya ajira iliyo wazi, ateuliwe mtu rnwenye sifa na kuijaza kutoka ndani ya Kampuni. Endapo atakosekana mfanyakazi mwenye sifa, nafasi hiyo itangazwe kwa wote.

7.2 Uchunguzi wa Kiafya kwa Ajili ya Ajira

Mtu yeyote anayetegemea kuajiriwa na Kampuni hataruhusiwa kuajiriwa kabia hajafanyiwa uchunguzi wa kiafya katika hospitali inayotambuiiwa na Kampuni. Iwapo Kampuni haitaridhika, ina haki ya kurudia uchunguzi huo. Gharama zote za uchunguzi zitalipwa na Kampuni.

8.0. AJIRA YA MKATABA

Mfanyakazi aliyestaafu na kupewa haki zake zote, au Mfanyakazi mwingirie kutoka nje ya Kampuni, hatapewa ajira ya mkataba kwa kuziba pengo ambalo linaweza kujazwa na Mfanyakazi aliyepo kazini.

9.0. LUGHA RASMI

Lugha rasmi itakayotumika katika Kampuni ni Kiswahili na Kiingereza.

10.0 TAARIFA KWA MFANYAKAZI.

Mara baada ya kuajiriwa, Mfanyakazi atapewa habari zote muhirnu kuhusu ajira yake kwa maandishi.

11.0 SAA. ZA KAZI

11.1 Wafanyakazi wa kazi za zamu watapangiwa zamu kwa mzunguko katika siku yoyote kwa juma kutoka Jumatatu hadi Jumapili i.limradi Mfanyakazi rnhusika atastahili siku moja ya mapumziko kwa juma.

11.2 Hakuna Mfanyakazi yeyote atakayebadili saa alizoparigiwa kufanya kazi, kubadilisha zamu za kazi kati ya mtu na mtu au kutpkuhudhuria kazini bila ruhusa ya Msimamizi wa Kazi/Kitengo.

11.3 Saa za kufanya kazi ni zile ambazo zimekubalika kisheria na zitazingatia Sheria zilizopitishwa na Bunge juu ya jurrila ya saa za kazi katika siku na juma na Mikataba ya Kimataifa iliyoridhiwa na Serikali.

11.4 (a) Iwapo Mfanyakazi atatakiwa kufanya kazi zaidi ya saa za kawaida atastahili kulipwa malipo ya saa za ziada (Overtime).

(b) Malipo ya saa za ziada yatakuwa kutokana na Sheria ya Ajira iliyopo mara moja na nusu ya malipo katika siku za kawaida, na mara mbili ya malipo ya kutvya ya siku za mapumziko na siku kuu.

(c) Kutokana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Mwajiri.atamlipa Mfanyakazi angalau asilirnia tano (5%) ya mshahara halisi wa mfanyakazi kwa kila saa aliyofanya usiku na kama masaa aliyofanya ni ya masaa ya ziada asilirnia tano itakokotolewa katika kiwango cha malipo ya ziada ya mfanyakazi.

12.0 UTOAJI TAARIFA YA KUACHA AU KUACHISHWA KAZI

12.1 Mfanyakazi yeyote wa kudumu mwenye nia ya kuacha kazi, atatakiwa kutoa taarifa ya miezi mitatu (3) ya kuabha kazi. Kampuni pia itatoa taarifa ya muda huo huo endapo inakusudia kumwachisha kazi Mfanyakazi wa kudumu.

12.2 Iwapo Kampuni au Mfanyakazi atashindwa kutoa taarifa (notisi) ya miezi mitatu kwa upande mwingine, upande unaohusika utalipa mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi..

12.3 Taarifa ya kuacha au kuachishwa kazi inaweza kutolewa wakati wowote kulingana na taratibu ziiizopo, na tarehe ya utoaji notisi itakuwa ndani ya kipindi cha utoaji wa taarifa hiyo.

12.4 Kutegemea uamuzi wa Mwajiri, taarifa ya kuacha kazi haiwezi ikabadilishwa au kufutwa mara itakapopokelewa kimaandishi. .

12.5 Malipo yote anayostahili anayeacha au kuachishwa kazi yatafanyika katika kipindi cha miezi mitatu ya taarifa.

13.0 MASHAURI YA KINIDHAMU

13.1 Iwapo Mfanyakazi atatuhumiwa kutenda kosa la kinidhamu shauri lake litashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi na au kwa kanuni za nidhamu za Kampuni kama ilivyo katika kiambatanisho Na. 1 (Annexure 1} cha Mkataba huu.

13.2 Mashauri ya kinidhamu yanayowakutariisha Mwajiri na Mfanyakazi maamuzi yake yasichukue zaidi ya siku 90 taka Mfanyakazi kupewa barua ya tuhuma isipokuwa kwa kesi za Jinai ambazo maamuzi yake hutegemea Mahakama.

14.0 KUPANDISHWA DARAJA

14.1 Utambuzi wa mtu rnwenye sifa za kupanda cheo/daraja utazingatia elirnu, stadi, utendaji kazi, uwezo na utumishi wa muda mrefu katika Kampuni.

14.2 Mfanyakazi aliyepandishwa daraja atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi sita (6).

14.3 Mfanyakazi ambaye atapandishwa daraja, kwa kuanzia atalipwa kiwango cha chini cha mshahara, katika daraja lake jipya, kinachozidi mshahara wake wa daraja la zamani.

14.4 Mfanyakazi yeyote atakayekataa kupandishwa daraja bila ya kuwa na sababu za msingi, hatafikiriwa kupandishwa cheo mpaka hapo waiiokuwa katika daraja hilo kwa wakati huo watakapokuwa wamepandishwa.

15.0 UTEUZI WA KUKAIMU

15.1 Mfanyakazi anaweza kukaimu nafasi ya juu kwa taratibu zifuatazo:-

(a) Uteuzi wa kukaimu kwenye nafasi iliyo wazi mdja kwa rnoja (permanently vacant), usiozidl miezi sita (6). Kama-utazidi hapo, itabidi Mfanyakazi athibitishwe katika nafasi hiyo.

(b) Nafasi ya kukaimu kwa ajili ya kufanikisha shughuli za utawala (administrative convenience) liazima iwe katika maandishi ya uteuzi huo.

(c) Uteuzi wowote wa kukaimu uwe wa maandishi.

15.2 Mfanyakazi yeyote atakayetaldwa kukaimu kutokana na kifungu kidogo cha 15.1 atakuwa na haki ya kulipwa stahili zifuatazo;baada ya kutimiza siku kumi na nne (14) mfululizo.

(a) Malipo ya majukumu ya nafasi ya Mkaimu yatalipwa kutokana na kanuni ziiizopo.

(b) Posho ya kukaimu, itakuwa ni tofauti kati ya mshahara wa Mkaimu na kiwango cha chini cha ngazi ya mshahara wa Mkaimiwa. Iwapo kiwango cha chini cha ngajd ya mshahara wa Mkaimiwa kitakuwa c'hini ya mshahara wa Mkaimu, posho hiyo itakuwa ni tofauti kati ya mshahara wa Mkaimu wa kiwango cha chini cha mshahara, katika ngazi ya Mkaimiwa, kinachozidi mshahara wa Mkaimu.

15.3. Mfanyakazi yeyote atakayeteuliwa kukaimu atazingatia na kuheshimu saa za kazi, masharti ya kazi, mazingira na hali ya kazi kulingana na nafasi aliyopewa kukaimu

16.0 UHAMISHO

16.1 Mfanyakazi yeyote anaweza kuhamrshwa rnoja kwa moja au kwa muda toka kituo kimoja hadi kingine. Uhamisho huo utasitishwa pale mwajiri atakaporidhika na matatizo ya mfanyakazi.

16.2 Mfanyakazi yeyote atakayekataa uhamisho unaoambatana na kupandishwa cheo (Transfer on Promotion), kwa sababu zake binafsi, atakuwa amepoteza haki yake ya “Promotion” hiyo.

16.3 Mfanyakazi am.baye ni kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Mwenyekiti, Katibu wa-Tawi na Mwenyekiti wa Kanda) iwapo atatakiwa kuhamishwa nje ya eneo lake la uongozi uhamisho ambao si kupanda Daraja, Menejiment itafanya mashauriano na Chama cha Wafanyakazi ngazi ya Taifa.

17.0 LIKIZO

17.1 Likizo ya mwaka itakuwa siku ishirini na nane (28) na itatolewa kufuata siku za kalenda.

17.2 Likizo ya mwaka itatolewa kwa Mfanyakazi baada ya kutimiza miezi kumi na miwiii kazini tangu kuajiriwa. Mfanyakazi, mke/mume na watoto au wategemezi wanaotambuiika kisheria ili mradi idadi yao isizidi wanne, watastahili tiketi moja (1) (return ticket) au nauli kwa wale ambao wanatoka sehemu ambkzo hazina huduma za roll kwa mwaka katika daraja analostahili Mfanyakazi.

17.3 Limbikizo la likizo halitazidi mara mbili ya stahili ya likizo ya mwaka, isipokuwa kama kuna sababu maalum. Likizo italimbikizwa zaidi ya stahili ya miaka miwiii pale tu ambapo imeombwa na Mfanyakazi na kuzuiwa na Mwajiri kimaandishi.

17.4 Mfanyakazi anavf/eza kubadili muda wa likizo yake kwa kuandika barua ya maombi kwa Mwajiri. Hata hivyo maombi yatategemea uamuzi wa Mkurugenzi Mtendaji kwa kuzingatia hali ya kazi na uwezo wa kifedha katika Kampuni.

17.5 Mfanyakazi yeyote anayechukua likizo'isiyopungua siku kumi na tano (15), anaweza kuchukua malipo badala ya likizo, kwa kiwango kisichozidi siku hamsini na sita (56) katika siku zake zilizosalia, kutegemea na uamuzi wa Mkurugenzi Mtendaji.

17.6 Mfanyakazi yeyote ambaye likizo yake ya mwaka itakataliwa, siku zake za likizo zitalimbikizwa kulingana na kifungu cha 17.3 hapo juu.

17.7 Likizo inaweza, kutolewa kwa idhini ya Mkurugenzi Mtendaji au Kiongozi yeyote aliyepewa mamlaka hayo na Mkurugenzi Mtendaji. Na kwa mamlaka’yake anaweza kukubali, kubadilisha, au kuahirisha kulingana na hali ya Kampuni.

17.8 Mfanyakazi yeyote ambaye amepata likizo kutokana na kifungu 17.1 na anaendelea na likizo, ana haki ya marupurupu kama ilivyoelezwa kwenye kifungu Na. 17.2 cha makubaliano haya.

18.0 LIKIZO-YA UZAZI

18.1 Mfanyakazi wa kike anjibaye ametimiza muda wa rnajaribio wa miezi kumi na mbili (12) atastahili kupata likizo ya uzazi ya siku themanini na nne (84) yenye malipo ya mshahara. Mfanyakazi atakayejifungua kabla ya kumaliza kipindi cha majaribio cha miezi kumi na mbili (12) hatastahili iikizo ya uzazi, i!a anaweza kuomba na kupewa Iikizo bila malipo isiyozidi siku themanini na nne (84). Likizo ya uzazi haiwezi kuuzwa.

18.2 Likizo ya uzazi itatoiewa mara moja baada ya miaka mitatu.

18.3 Iwapo Mfanyakazi war;kike atajifungua mtoto aliyekufa au ambaye atafariki katika kipindi cha mwaka mmoja tangu azaliwe, Mfanyakazi huyo atastahili kupata likizo nyingine ya uzazi kabla ya kutimiza miaka mitatu (3).

18.4 Iwapo mke wa mfanyakazi atajifungua mtoto, mfanyakazi atastahili likizo ya siku tatu (3) kwa mujibu'wa kifungu 18.1 hadi 18.3 cha Mkataba huu.

19.0 LIKIZO YA HURUMA (COMPASSIONATE LEAVE)

Katika matukio ya kifo cha rnkqi au mume wa mfanyakazi au mtoto, mlegernezi au mzazi wake, mfanyakazi atastahili kupewa likizo ya huruma isiyozidi siku kumi na line (14). Likizo hii haitakuwa sehemu ya likizo ya kawaida ya mfanyakazi kwa mwaka huo.

20.0 LIKIZO YA DHARURA (EMERGENCY LEAVE)

Likizo ya dharura isizidi siku kumi na nne (14), na likizo hii haihusishi malipo yoyote ya usafiri. Likizo hii itakuwa sehemu ya likizo ya mwaka ya Mfanyakazi.

21.0 MADARAJA YA USAFIRI

Mfanyakazi atastahili usafiri wa Madaraja kama ifuatgvyo:

•TRD 1-TRD 6, TRC 1-TRC 5 na TRB 1-TRB 2 Daraja la Pili Kulala.

•TRC 6, TRB 3-TRB 6, TRA 1 -TRA 8 Daraja la Kwanza.

22.0 MARUPURUPU

22.1 Malipo ya Kujikimu

Mfanyakazi anapokuwa- katika safari za kikazi, malipo yake ya kujikimu yanayohusisha malazi na chakula yatafuata rnuundo utakaowekwa na mwajiri akizingatia ngazi ya Mfanyakazi na.mahali panapohusika, Viwango vya malipo ya kujikimu vitabadilishwa kila inapobidi kulingana na gharama za maisha na hali ya Kampuni kifedha. Kwa wakati huu, muundo na viwango vitakuwa kama ifuatavyo:-

ENEO TRA 7 - 8 TRA 5(R) -6 TRA 3 - 4 TRA 3R-4R TRA 1— 2

TRB 5-6

TRA 1R - 2R

TRB 5R - 6R

TRB 1 - 4

TRB 1R-4R

TRC 1 - 6

TRD 1 - 6

Manispaa/Jiji

Mji Mkuu wa Mkoa na Wilaya

Mji Mdogo na Vijiji

Safarini (On Transit)

80,000/=

75,000/"

70,000/=

20,000/=

75,000/=

70,000/=

50,000/=

20,000/=

70,000/=

60,000/=

40,000/=

20,000/=

50,000/=

40,000/=

80,000/=

20,000/=

45,000/=

30,000/=

25,000/=

20,000/“

(a) Wafanyakazi wapya wanaokwenda kuanza kazi watastahili kulipwa fedha ya kujikimu siku kumi na nne (14).

(b) Shirika halitalipa marupurupu ya kujikimu kwa Mfanyakazi yeyote ambaye anasafiri toka kituo chake cha kazi. kwenda likizo au anaporudi kutokajikizo au kwa Mfanyakazi aliyesimamishwa kazi.

(c) Mfanyakazi anayehamishwa kutoksi Kituo kimoja hadi kingine atalipwa marupurupu ambayo angelipwa wakati akiwa safarini kikazi. Kama atasafiri na familia yake atalipwa yeye na mke wake marupurupu yaliyo sawa. Iwapo atasafiri na watoto wake na wengine wanaomtegemea-kisheria wasiozidi wanne walio chini ya miaka kumi na nane (18) au walioko katika masomo ya Sekondari watalipwa nusu ya marupurupu alipwayo Mfanyakazi.

(d) Mfanyakazi anayehamishwa na Kampuni haijampatia nyumba atastahili kupata huduma zifuatazo:-

(i) Posho ya Kujikimu kwa siku ishirini na moja (21)

(ii) Kwa Mfanyakazi ambaye kutokana na ngazi yake ya kazi, anastahili kupewa nyumba na Mwajiri, atastahili kulipiwa pango la hoteli inayolingana na hadhi yake kwa siku kumi na nne (14), Kampuni itamlipia gharama za malazi na chakula (Full Board); au achague kupewa posho ya kujikimu kwa siku kumi na nne (14).

22.2 Uhamisho wa Kudumu

(a) Mfanyakazi anapojiandaa kwa uhamisho kutoka kituo kimoja hadi kingine, nje ya kituo chake cha kazi; atastahili kulipwa marupurupu ya usumbufu au posho ya usumbufu kwa kutumia kiwango cha mshahara wake wa rnwezi mmoja (basic salary).

(b) Mbali na malipo hayo hapo juu, Kampuni itakuwa na wajibu wa kulipa gliarama za kufunga mizigo sawa ha shilingi Jaki rnoja na elfu hamsini (Shs. 150,000/=) au shilingi laki tatu (Shs. 300,000./=) kufuatana na figazi ya mshahara wa Mfanyakazi, kama ilivyoainishwa kwenye sera ya Kampuni kuhusu malipo hayo.

(c) Mfanyakazi atakayetakiwa kuhama toka kituo kimoja hadi kingine, atastahili kupewa siku mbili (2) moja ya kufunga mizigo na rnoja ya kufungua mizigo.

(d) Malipo ya uhamisho hayatalipwa iwapo uhamisho umeombwa na Mfanyakazi mwenyewe kutokana na sababu zake binafsi.

22.3 Kushikilia nafasi (Relieving duties)

Mfanyakazi ambaye anatakiwa na Kampuni kwenda kushikilia nafasi ya kazi, hatalipwa marupurupu ya uhamisho. Badata yake atalipwa posho ya

“Relieving Allowance” kwa siku zisizozidi thelathini (30) kwa viwango vinavyotumika kwa wakati huo, kwa kuzingatia yafuatayo:-

(a) Malipo ya kawaida ya posho ya kujikimu yanayolipwa kwa Mfanyakazi, pale arribapo Kampuni haitoi malazi wala chakula.

(b) Asilimia hamsini (50%) ya kiwango, cha kawaida cha posho ya kujikimu, pale ambapo Kampuni inatoa malazi tu bila chakula.

(c) Asilimia ishirini (20%) ya kiwango cha kawaida cha posho ya kujikimu, pale ambapo Karnpuni inatoa malazi na chakula.

(d) Iwapo Mfanyakazi atahitajika kuendelea kuwepo kwenye “Relieving Duties”'Zaidi ya siku thelathini (30) kwa idhini ya Mkurugenzi Mtendaji atastahili malipo kwa utaratibu ulioahishwa kwenye kifungu 22.3(a) – (d) ili mradi jumla yake isizidi siku tisini (90).

22.4 Uhamisho wa muda rnfupi (Temporary Transfer)

Mfanyakazi atakayekuwa nje ya kituo chake cha kazi kwa zaidi ya siku tisini (90) atahesabika kania yuko kwenye uhamisho wa muda. mfupi (Temporary Transfer), na atastahili rfialipo ya posho ya kujikimu ya siku therathini (30). inapozidi siku therathini (30), kibali kitaombwa kwa Mkurugenzi Mtendaji.

(a) Mfanyakazi anapokuwa katika Uhamisho wa muda mfupi, atalipwa posho ya kujikimu ya siku therathini (30), yeye peke yake ikiwa Mwajiri hatampa nyumba.

(b) Mfanyakazi anaweza kuwa kwenye uhamisho wa muda mfupi kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu (3).

(c) Baada ya miezi mitatu ya uhamisho wa muda mfupi, Mfanyakazi atastahili uhamisho wa kudumu, ikizingatiwa kwamba malipo ya uhamisho huu wa kudumu yatakuwa kwa ajili ya mke na watoto tu.

22.5 Posho ya Mavazi ya Safari (Outfit Allowance)

Posho ya mavazi ya, safari itatolewa kwa wafanyakazi wanaokwenda kazini/mafunzo nje ya nchi kwa kiwango cha shilingi laki tatu (300,000/=).

Posho ya mavazi italipwa mara moja kila baada ya miaka mitatu.

22.6 Posho ya Nyumba

(a) Kampuni itatoa posho ya nyumba kila mwezi kwa Mfanyakazi wake wa kudumu, ambaye hajapewa nyumba ya Kampuni, sawa na asilirnia kumi na saba (17%) ya mshahara wake wa mwezi.

(b) Inapowezekana, Mfanyakazi atapewa nyumba ya Kampuni. Mfanyakazi atakayepewa nyumba ya Kampuni hatalipwa waia kuiipa kodi ya pango. Iwapo yeye na mume/mke wake wote ni waajiriwa wa Kampuni, basi mmojawapo ndiye atastahili kupewa nyumba na mwenzake atastahili posho ya nyumba.

23.0 KUSTAAFU

23.1 Mfanyakazi atastaafu kwa mujibu wa sheria urnri wake wa kustaafu utakapofika. Mfanyakazi anaweza kustaafu endapo afya yake itaonekana hairnruhusu kuendelea na kazi yoyote na hali hiyo kuthibitishwa na Daktari anayetambulika na Kampuni au Bodi ya Madaktari.

23.2. Mfanyakazi anapostaafu na kama hajalipwa haki zake zote na kampuni kwa wakati au kwa muda ambao kampuni itakuwa haijakamilisha michango na kuwasilisha makato kwenye mifuko husika ya mwanachama, basi mfanyakazi huyo ataendelea kulipwa mshahara hadi hapo atakapolipwa mafao yake yote yanayotokana na kampuni, isipokuwa pale mfanyakazi atakapo kwepa kulipwa mafano.

23.3 Mfanyakazi atakayepatwa na hali kama inavyoelezwa kwertye kifungu 23.1,

23.2 na 23.6, ataendelea kuishi kwenye nyumba ya Kampuni mpaka hapo atakapolipwa stahili zake zinazolipwa na Kampuni.

23.3 Mstaafu hatastahili kuendelea kuishi kwenye nyumba ya Kampuni mara baada ya kupewa haki zote.

23.4 Mstaafu atastahili tiketi moja (Free Pass) kwa mwaka yeye na mke/mume wake.

23.6 Mstaafu atastahili Tuzo ya Kustaafu ya malipo ya mshahara (aliostafia) wa rnwezi mmoja kwa kila .mwaka kwa miaka yote ya utumishi wake.

24.0 UTENDAJ1 WA KIJAS1R1 (MERITORIOUS CONDUCT)

Mfanyakazi yeyote ambaye.amefanya kitendo cha ujasiri katika kuokoa maisha ya watu na mali ya Kampuni, taarifa yake ipelekwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni kwa kufikiriwa zawadi au tuzo inayostahili.

25.0 MICHEZO YA KUBAHATISHA NI MARUFUKU

Hairuhusiwi kuendesha aina yoyote ya michezo ya kubahatisha katika eneo la kazi,

26.0 KUJIWEKA KWENYE MAZINGIRA YA HATARI

Tahadhari ya hali ya juu Ichukuliwe kuzuia utokeaji wa ajali, Hairuhusiwi kwa Mfanyakazi yeyote kukaa katika mazingira ya hatari au kuwaweka Wafanyakazi wenzake katika mazingira ya hatari.

27.0 CHETI CHA UTUMISHI

Mfanyakazi yeyote anayeacha, anayeachishwa, kupunguzwa au anayestaafu kazi atapatiwa cheti cha utumishi na atakabidhiwa mafraf moja anapolipwa haki zake. Cheti hicho kitakuwa na maelezo yafuatayo:-

(a) Jina Ui Mfanyakazi;

(b) Jina la Mwajiri;

(c) Tarehe ya kuanza ajira;

(d) Aina ya kazi na cheo

(e) Kiwango cha mshahara na daraja alilofikia wakati wa kuacha kazi;

(f) Tarehe ya kuacha kaz,i;

(g) Sababu za kuacha kazi;

(h) Namba ya NSSF/PPF na Mamba ya kuajiriwa;

(i) Namba ya NSSF/PPF ya Kampuni.

28.0 MALI ZA TRL ZITAKAZORUD1SHWA WAKATI WA KUACHA KAZI

28.1 Mfanyakazi atakapoacha, atakapostaafu, atakapoachishwa au atakapopunguzwa kazi atatakiwa kurejesha mali na vifaa vyote vya Kampuni.

28.2 Iwapo kuna mali au vifaa vyovyote ambavyo havijarudishwa au vimeharibika kwa matumizi mabaya, gharama za vifaa hivyo au matengenezo zitakuwa ni deni la Mfanyakazi ambalo iitakatwa kwenye mafao yake.

29.0 ULEVI KAZINI

29.1 Ni marufuku kwa Mfanyakazi kutumia/kuwa na rnadawa ya kulevya, gongo, bangi au aina yoyote ya kileo akiwa kazini. Mfanyakazi atakayekiuka agizo hili atachukuliwa hatua za kisheria.

29.2 Ni marufuku kwa Mfanyakazi kuwa na aina yoyote ya kileo katika sehemu nyeti za Kampuni kama “Engine room", “Brake van”, "Control Office” na “Footplate".

29.3 Ni marufuku kwa Mfanyakazi kuwa kazini akiwa amelewa. Ulevi utathibitishwa kwa kutumia vipimo maalurn an kwa kufuata taratibu nyingine ambazo Kampuni inazitumia kwa wakati huu, kama kuthibitisha ulevi mbele ya mashahidi. Mfanyakazi atakayekataa kupimwa au kuthibitishwa mbele ya mashahidi atahesabika kuwa amelewa.

30.0 POSHO YA KUJIKIMU KWA MFANYAKAZI AMBAYE AN AT AKIWA KUTOA USHAHIDI

Mfanyakazi ambaye ameitwa kutoka kwenye kituo chake cha kazi kutoa ushahidi kwa mashauri yanayohusiana na Kampuni, atalipwa fed ha ya kujikimu kama iiivyo katika kanuni za kazi za Kampuni zilizopo. Posho hii italipwa pale tu arnbapo Mahakama au sehemu husika.ya kutolea ushahidi haitoi malipo hayo

31.0 TUZO YA UTUMISHI WA MUDA MREFU

31.1.Mfanyakazi anayestaafu au familia ya Mfanyakazi aliyefariki ambaye alitimiza masharti ya tuzo ya muda mrefu atastahili kupata tuzo ya utumishi wa muda mrefu kwa viwango vifuatavyo:

MUDA WA UTUMISHI MABATI G.30 MITA 3 CEMENTI MIFUKO
(i)

(ii)

(iii)

(iv)

Miaka 16-20

Miaka 21 --25

Miaka 26 – 30

Zaidi ya miaka 30

50

60

80

100

50

50

50

50

Hata hivyo malipo ya mabati yatalipwa kwa kiasi kitakachobaki baada ya kutoa yaliyokwisha kulipwa wakati wa TRC. Hii itakuwa kwa wafanyakazi waliolipwa.

31.2 Iwapo Mfanyakazi atapunguzwa kazini tuzo'hiyo itaanzia miaka 15 badala ya 16.

31.0 UKAGUZI WA MAJALADA BINAFSI

32.1 Mfanyakazi haruhusiwi kushughulikia au kulikagua jalada lake .binafsi. Barua za mapendekezo au za kinidhamu zinazomhusu Mfanyakazi zitatunzwa katika jalada lake binafsi. Hainan hizo zitatolewa kwa Mfanyakazi kimaandishi.

32.2 Mfanyakazi yeyote atakayekiuka utaratibu kwenye kifungu 32.1 hapo juu, atachukuliwa hatua za kinidhamu.

32.2 VITAMBUHSHO

Kampuni itatoa kitambulisho kwa kila Mfanyakazi wake ambacho atatakiwa kukionyesha kila itakapompasa kufanya hivyo. Katika mtukio ambayo Mfanyakazi anakosa kitambulisho, kwa kupoteza au kwa mazingira yoyote yale, anatakiwa atoe taarifa kwa rrisimamizi wake ili apewe kitambulisho kingine. Kama itadhihirika kwamba kupotea kwa kitambulisho hicho kumesababishwa na uzembe wa mhusika, gharama za kitambulisho kipya zitakuwa juu ya Mfanyakazi mwenyewe.

34.0 MALI ZA TRL ZlSITUMlKE KWA SHUGHULI ZA BINAFSI

MTanyakazi yeyote haruhusiwi kutumia au kuhamisha chombo au rnali ya Kampuni kwa shughuli binafsi ila kwa idhini maalurri kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji.

35.0 MAONI YA WAFANYAKAZI

Kila Mfanyakazi anayo haki ya kuwasiiisha kwa Mwajiri maoni yake au rnawazo yoyote yenye kuongeza ufanisi kwa Kampuni au kuimarisha mazingira salama ya kazi.

36.0 MALIPO YA MSHAHARA KATIKA HALI AMBAYO UTHIBITISHO WA UWAKALA. UTATOLEWA AU NYARAKA ZINAWEZA KUTOLEWA NA MFANYAKAZI

36.1 Mshahara utalipwa kwa Mfanyakazi mwenyewe isipokuwa katika mazingira yafuatayo:

(a) Mfanyakazi hakuwepo katika kituo chake cha kawaida cha malipo, au hakuwepo kituoni kwa sababu ya likizo, au hakuwepo kituoni kwa sababu za ugonjwa ambazo zinathibitishwa na Mganga anayetambulika

(b) Makato ya kisheria, kama kodi ya mapato, yatapunguzwa kutoka kwenye mshahara wa Mfanyakazi.

36.2 Kutokana na mazingira yaliyoelezwa kwenye kifungu 36.1(a), Mfanyakazi anaweza kuchukuliwa mashahara wake na mtu mwingine kama mfanya kazi atatoa idhini ya kulingana na utaratibu uliowekwa na Mwajiri. Mfanyakazi atatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi tena ili kubadili mlipwji kuwa yeye mwenyewe

36.3 Katika mazingira yeyote, hairuhusiwi mtu a'liyepewa' idhini ya kuchukua mshalfara wa Mfanyakazi kutoa idhini nyingine kwa mtu wa tatu kuchukua mshahara huo.

37.0 UFARAGHA MAENEO NYETI

Mtu yeyote asiyehusika na eneo, mahali,.chumba au ofisi nyeti (kama vile Chumba cha kuchapisha au kukatisha tiketi, “Cash Office”, Chumba cha Mawasiliano ya Simu, “Computer Room” “Signalling Relay Room”, Carrier Room”, “Control Room”, Masijala, Ndani ya Kichwa cha Treni, “Brake Van) hataruhusiwa kuingia katika sehemu hizo, isipokuwa kwa ruhusa maalum.

38.0 POSHO YA USAFIRI

Kampuni itatoa posho ya usafiri sawa na shilingi elfu thelathini (Shs. 30,000/=) kwa mwezi kwa Wafanyakazi wa Kampuni kuanzia ngazi ya TRD 1 hadi TRA 2. Hata hivyo Kampuni na TRAWUwatatafuta utaratibu wa kuingiza posho hiyo katika mishahara ya Wafanyakazi.

39.0 KIFO CHA MFANYAKAZI, MKE/MUME

39.1 Katika tukio la kifo cha Mfanyakazi, mkewe au mumewe, Kampuni itamlipa mfiwa anayetambuliwajumla ya shilingi laki tano (Shs. 500,000/=) kama rambirambi (Pole na Sanda).

39.2 Mfanyakazi aliyefiwa na mume/mke, mtoto na wazazi atapewa tiketi ya treni ya kurudi ya staili yake pale penye usafiri wa Reli. Endapo hakuna usafiri wa Reli na akatumia basi atarudishiwa nauli.

40.0 KIFO CHA MTOTO, BABA, MAMA AU MTU ANAYEMTEGEMEA MFANYAKAZI

Katika tukio la kifo cha mtoto wa kuzaa Mfanyakazi, mama, baba, au mtu anayemtegemea Mfanyakazi, ambaye anatambulika kisheria, Mwajiri atatoa kiasi cha shilingi laki tatu (Shs. 300,000/=) kama rambirambi (Pole na Sanda). Mwajiri pia atagharamia sanduku/ubao pamoja na usafiri mpaka sehemu ya mazishi ndani ya Tanzania. Sehemu ya mazishi itaamuliwa na wafiwa.

41.0 KUMRUDISHA MFANYAKAZI KWAO

41.0(A)

Kama Mfanyakazi atafikia muda wa kustaafu, kupunguzwa, kuacha au kuachishwa kazi, Mwajiri atalipa gharama za kufunga mizigo na kumrudisha nyurnbani anakotoka. Mwajiri atamsafirisha katika daraja alilostahili akiwa rntumishi. Hii ni pamoja na familia yake na mizigo yake kama ifuatavyo:-

MADARAJA UZITO FEDHA ZA KUFUNGA MIZIGO
TRD 1 - TRD 6

TRC 1 - TRC 2

Tani 2 Shs. 150,000/=

TRC 3 - TRC 6

TRB 1 - TRB 6

TRA 1 - TRA 8

Tani 4

Shs: 300,000/=

41.0 (B)

GHARAMA ZA KUSAFIRISHA MIZIGO

Kampuni itagharamia usafirishaji wa mizigo kwa kiwango cha shs. 1,000/- kwa tani 1 kwa kilomita 1. Kampuni itakuwa ikihuisha viwango hivi kulingana na maelekezo ya Serikali.

42.0 KUPUNGUZWA KAZI (REDUNDANCY)

Sera ya Nchi ni kuongeza na.kulinda ajira. Katika hali hiyo, Mwajiri anatambua umuhimu wa matumizi bora ya Wafanyakazi kama ndio njia pekee ya kulinda ajira. Mata hivyo, inaweza kutokea kwamba Mwajiri ' anaiazimika kupunguza Wafanyakazi. Katika haii hiyo, Mwajiri atafanya rnajadiliano na TRAWU kupitia Baraza Kuu la Majadiliano, na kuchukua hatua zifuatazo, si chini ya miezi mitatu kabla ya upunguzaji wa Wafanyakazi.

(a) (i) Kuacha kuajiri Wafanyakazi wa muda (Contract Staff) katika fani

na ngazi zinazohusika;

(ii) Kuacha kuajiri Wafanyakazi wapya katika nafasi zinazohusika;

(iii) Kuangalia uwezekano wa kuwahamishia Wafanyakazi wazuri katika sehemu nyingine za kazi ndani ya Kampuni (Redeployment);

(iv) Kutoa mafunzo ya ujuzi na ustadi unaohitajika (Retraining) na kwa wafanyakazi waliohamishiwa kwenye sehemu nyingine ambazo hawana ujuzi nazo.

(b) Baada ya hayo yote hapo juu kufanyika, basi kifungu 38 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na 6 ya mwaka 2004 itabidi kifuatwe kukamiiisha

zoezi zima la upunguzaji (redundancy) kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

(i) Waliofikia umri wa miaka hamsini na tano (55) au zaidi.

(ii) Wenye afya mbaya ambayo uthibitisho wa vyeti vya Matibabu na taarifa ya Daktari utatumika katika kufikia uamuzi.

(iii) Watakaoomba wenyewe kupunguzwa (wakikubaliwa na Menejimenti).

(iv) Wenye nidhamu mbaya kama itakavyoonekana kwenye mafaili yao na kuthibitishwa na viongozi wa matawi husika.

(v) Wale ambao Vitengo/Nafasi zao zimefutwa

(vi) Waliosimamishwa, kazi zaidi ya miaka miwiii ambao watahesabika wako kazini tangu tarehe ya kusimamishwa kazi.

(c) Hata hivyo, zitaangaliwa sababu nyingine, hasa aina ya majukumu ya Mfanyakazi, na kumuondoa Mfanyakazi ambaye haimudu kazi, hana nidhamu au hazalishi.

(d) Baada ya kutumia vigezo vilivyoelezwa katika kifungu cha 42 (b) (i-vi) na (c) na bado ikaonekana kuwa upunguzaji wa Wafanyakazi bado unahitajika. Wafanyakazi wa ngazi moja watapunguzwa kwa kuzingatia kigezo cha waliotangulia kuajiriwa watakuwa wa mwisho kupunguzwa “Last In, First Out” (LIFO).

43.0 MALIPO YA KUPUNGUZWA KAZI:

43.1 Viwango vya malipo/mafao kwa wale watakaopunguzwa kazi vita kuwa kama ifuatavyo:-

(a) Mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi

(b) Nauli ya kurudi nyumbani kwa Mfanyakazi na famiiia yake na mizigo kulingana na stahili ya Mfanyakazi.

(c) Limbikizo la likizo zote ambazo Mfanyakazi aliomba na kuzuiliwa na uongozi kutokana na majukumu ya Kampuni.

(d) Kiinua Mgongo kwa wale wanaohusika na Sheria hiyo.

(e) Kwa wale Wanachama wa NSSF na PPF watalipwa mafao yao na mifuko husika.

43.2. Mfanyakazi aliyehamishiwa kwenye Kampuni na akapunguzwa atalipwa pia kama ifuatavyo:-

(a) Mkono wa Heri

(i) Mishahara ya miezi arobaini (40) katika ngazi ya TRD 1 -

TRD 6 na TRC 1 - TRC 2.

(ii) Mishahara ya miezi thelathini na tano (35) katika ngazi ya

TRC 3 - TRC 6 na TRE3 1 - TRB 3.

(iii) Mishahara ya miezi thelathini (30) katika ngazi ya TRB 4 - TRB 6.

iv) Mishahara ya miezi ishirini (20) kaika ngazi ya.TRA 1 - TRA 8.

b) Mafao mengineyo (Other Benefits)

Posho ya Nyumba

Posho ya nyumba ya asilirnia kumi na saba (17%) itaendelea kutolewa kwa Mfanyakazi aliyepuriguzwa kwa kipindi cha. miezi mitatu (3). Kwa Mfanyakazi anayeishi kwenye nyumba ya Kampuni ataendelea kuishi kwenye nyumba kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu (3) baada ya kupunguzwa.

43.3 Mfanyakazi aliyepunguzwa na kama hajalipwa choehote katika haki zake na Kampuni, basi Mfanyakazi huyo ataendelea kulipwa mshahara hadi hapo atakapolipwa mafao yake na gharama za usafiri zinazotokana na Kampuni isipokuwa pale Mfanyakazi atakapokwepa kulipwa mafao.

44.0 KUHAMA AJIRA

44.1 Iwapo Mfanyakazi aliyepo kazini atahamishiwa kwa mwajiri mwingine ajira yake itaendelea kutambuiiwa tangu alipoajiiiwa kabla ya kuhamishiwa kwa Mwajiri huyo kama ilivyoelezwa kwenye Sheria, ya Reli Na. 4 ya mwaka 2002. Mafao na maslahi yake nayo yataendelea karrta yalivyo katika Mkataba huu.

44.2 Iwapo mwajiri mpya atasimama kuenclesha shtighuli za reli kwa sababu yeyote ile, Serikali au Mamlaka yeyote itakayopewa jukumu la kuendesha shughuli za reli, itakuwa na wajibu wa kufekeleza yote yaliyomo ndani ya Mkataba huu.

45.0 MATIBABU

Kampuni itagharimia matibabu kwa Mfanyakazi mke/murne na watoto pamoja na wategemezi wasiozidi wanne wanaotambuliwa kisheria. Na pale ambapo hakuna Hospitali ya Kampuni, Kampuni itagharimia matibabu hayo ndani na nje ya nchi.

46.0 MAFUNZO YANAYO IDHINISIHWA NA TRAWU

Mfanyakazi ambaye, kwa idhini ya Mkurugenzi Mtendaji, atahudhuria mafunzo, vikao vya Vyama vya Wafanyakazi au semina iliyoidhinishwa na TRAWU, atahesabika kuwa yuko kazini katika kipindi chote cha, rnafunzo au semina hiyo

47.0 WADI YA MFANYAKAZI BORA

Kutokana na ushauri wa TRAWU, Baraza la Majadiliario la Wilaya na Kamati ya Utendaji ya Menejimenti ya Kampuni, Wafanyakazi Bora wawili (2) wa Ki-Wilaya watapewa cheti na zawadi ya Shilingi laki sita (Shs. 600,000/=) kila mmoja. Mfanyakazi wa Ki-Taifa atapewa cheti na zawadi ya Shilingi Millioni mbili (Shs. 2,000,000/=)

48.0 KATABA WA UWAKALA (AGENCY SHOP AGREEMENT

Kampuni na TRAWU watafanya mkataba wa uwaka1a (Agency Shop Agreement) chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini No. 6, 2004 kifungu No. 72 (2).

49.0 LIKIZO BILA MALIPO KWA VIONGOZI WA CHAMA (TRAWU)

(i) Mfanyakazi atakayechaguliwa au kuteuliwa kwa kazi za Chama (TRAWU) ambazo ni za utendaji wa kila siku (full time duties) mfano Katibu Mkuu au Naibu -Katibu Mkuu atahesabiwa kuwa yupoMikizo bila malipo mpaka pale atakapokuwa ameacha nafasi hiyo.

(ii) Mfanyakazi aliyemaliza kipindi chake cha-utumishi ambacho kinaelezwa katika kifungu cha (i) atarudishiwa daraja lake- aliloliacha wakati alipoteuliwa/kuchaguliwa katika nafasi hiyo. Endapo nafasi aliyokuwa nayo ama inayofanana ipo atarudishwa kazini.

50.0 POSHO YA MILEAGE (MILEAGE ALLOWANCE)

“Running staff” watastahili kuIipwa posho ya shilingi kumi na tano (I5/=) kwa kila kilomita moja itakayofanyiwa kazi. Malipo hayo yataingia kwenye mshahara.

51.0 MALENGO NA TIJA

51.1 Kampuni itaweka malengo na mipango yake ya kazi na kuyapitisha katika Baraza Kuu la Wafanyakazi ambalo litaishauri Bodi ya Wakumgenzi. Baada ya kukamilika Menejimenti ya Kampuni na TRAWU watakuwa na jukumu la kuwaelimisha Wafanyakazi wa ngazi zote kuhusu malengo, mipango na mikakati ya utekelezaji kama ilivyo kwenye kiambatisho Na. 2 cha Mkataba huu.

51.2 Kampuni itakuwa inawapa taarifa ya utekelezaji (Performance Report) Wafanyakazi kupitia matawi yao ya TRAWU kila baada ya miezi sita (6).

51.3 Kampuni na TRAWU watashauriana na kuweka mipango mizuri ya motisha ambayo itakuwa kichocheo cha ufanisi wa kazi.

51.4 Menejimenti ya Kampuni na TRAWU kwa pamoja wataweka mikakati itakayohakikisha kuwa aina zote za wizi na; ubadhilifu wa mail za Kampuni na wateja unazuiwa kadri iwezekanavyo ill kuimarisha uwezo wa Kampuni kifedha.

52.0 KUREKEBtSHA AU KUFUTA MKATABA HUU

52.1 Mkataba huu utafanyiwa marekebisho au kufutwa kabisa kwa makubaliano ya pande zote mbili. Taarifa ya kusudio la kurekebisha au kufuta Mkataba huu itatolewa kwa maandishi katika kipindi kisichopungua miezi mitatu (3) kwa kila upande.

52.2 Mkataba huu utaendelea kutambulika na pande zote zinazohusika hata kama Mwajiri atabadilika hadi hapo Mkataba'mwingine utakapofungwa ili kuendeleza mahusiano mazuri, ufanisi na arnahi kazi (Industrial harmony).

52.3 Miezi site kabla ya Mkataba kumalizika pande zote mbili zitakaa na kujadiliana juu ya Mkataba mpya na katika muda wote Wa majadiliano Mkataba huu utaendelea kuturnika na kuheshimiwa hadi hapo Mkataba mpya utakapokuwa umesainiwa.

KWA HIYO, Ufungaji na Makubaliano ya Mkataba huu kwa pande zote mbili zilizotajwa hapa chini yamefanyika hapa Dar es Salaam leo tare 29 Mwezi 02 Mwaka 2012

Jina ……………………………………………………………

Sahihi …………………………………………………………

Cheo/Wadhifa: MWENYEKITI WA BODI KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL)

Jina …………………………………………………………….

Sahihi …………………………………………………………..

Cheo/Wadhifa: MKURUGENZI MTENDAJI – KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL)

Jina ……………………………………………………………

Sahihi …………………………………………………………

TZA Kampuni Ya Reli Tanzania (TRL) - 2011

Start date: → 2011-03-10
End date: → 2013-03-09
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → 2012-02-29
Name industry: → Transport, logistics, communication
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Name company: →  Kampuni Ya Reli Tanzania (TRL)
Names trade unions: →  TRAWU - Chama Cha Wafanyakazi Wa Reli Tanzania

WORK AND FAMILY ARRANGEMENTS

Maternity paid leave: → 12 weeks
Maternity paid leave restricted to 100 % of basic wage
Job security after maternity leave: → Yes
Prohibition of discrimination related to maternity: → No
Prohibition to oblige pregnant or breastfeeding workers to perform dangerous or unhealthy work: → 
Workplace risk assessment on the safety and health of pregnant or nursing women: → 
Availability of alternatives to dangerous or unhealthy work for pregnant or breastfeeding workers: → 
Time off for prenatal medical examinations: → 
Prohibition of screening for pregnancy before regularising non-standard workers: → 
Prohibition of screening for pregnancy before promotion: → 
Facilities for nursing mothers: → No
Employer-provided childcare facilities: → No
Employer-subsidized childcare facilities: → No
Monetary tuition/subsidy for children's education: → No
Paternity paid leave: → 3 days

EMPLOYMENT CONTRACTS

Part-time workers excluded from any provision: → 
Provisions about temporary workers: → 
Apprentices excluded from any provision: → 
Minijobs/student jobs excluded from any provision: → 

WORKING HOURS, SCHEDULES AND HOLIDAYS

Working hours per day: → 8.0
Working days per week: → 6.0
Paid annual leave: → 28.0 days
Paid annual leave: → 4.0 weeks
Rest period of at least one day per week agreed: → Yes
Provisions on flexible work arrangements: → 

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Adjustment for rising costs of living: → 0

Premium for evening or night work

Premium for evening or night work: → 105 % of basic wage
Premium for night work only: → Yes

Premium for overtime work

Premium for overtime work: → 150 % of basic wage

Allowance for seniority

Allowance for seniority after: → 16 years of service

Meal vouchers

Meal allowances provided: → No
Free legal assistance: → 
Loading...