MAPENDEKEZO YA MKATABA WA HALI BORA BAINA YA TUICO KWA NIABA YA WAFANYAKAZI WA NYANZA BOTTLING CO. LTD NA MWAJIRI NYANZA BOTTLING CO. LTD TUICO 2013

New1

1.0 UTANGULIZI

Mkataba huu baada ya kukamilika kwake utakuwa ni mali ya CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA VIWANDA,BIASHARA,TAASISI ZA FEDHA HUDUMA NA USHAURI(TUICO) na NYANZA BOTTLING CO. LTD (NBCL).

2.0 UTAMBUZI

2.1 Chama cha Wafanyakazi TUICO kinatambua NBCL ndiye mwajiri ambaye wafanyakazi wake ni wanachama WATUICO.

2.2 Mwajiri anaitambua TUICO kuwa ndicho chombo pekee cha wafanyakazi kinachosimamia haki na maslahi yao.

2.3 Kila upande unatambua uhalali na uwepo wa chombo kingine na kwamba wafanyakazi ni kiungo kikubwa cha ushirikiano.

3.0 WAHUSIKA

Mkataba huu utawahusu wafanyakazi wote wa kiwanda hiki isipokuwa wataalamu toka nje.

4.0 KUDUMU NA TAREHE YA KUANZA MKATABA

4.1 Mkataba ukiisha sainiwa marekebisho yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa sheria.

4.2 Endapo Mkataba utakuwa umeisha muda wake utaendelea kuheshimika au kutumika hadi utakapopendekezwa Mkataba mpya na kusainiwa.

4.3 Mkataba huu utadumu kwa muda wa miezi 24

5.0 RIPOTI ZA WAFANYAKAZI

(i) Kutakuwa na ripoti za wafanyakazi za kila mwaka za maendeleo, na utendaji wa kazi zao ambazo kila Mkuu wa Idara atalazimika kuzijaza kumpelekea mwenye mamlaka ya juu.

6.0 MUDA WA MAJARIBIO

Pande zote mbili wamekubaliana kuwa atakayeajiriwa atakuwa na muda wa majaribio wa miezi mitatu. Baada ya muda huo kumalizika mwajiri atakuwa na haki ya kumwajiri au kumuachisha.

7.0 AJIRA

Pande zote mbili wamekubaliana kuwa kutakuwa na ajira za aina tatu:

(a) Ajira isiyokuwa na muda maalumu

(b) Ajira za muda maalum kwa wafanyakazi wa ngazi za uongozi na wataalamu

(c) Ajira ya kazi maalum

8.0 KUACHA/KUACHISHWA

8.1 Kwa sababu yoyote ile ya kimsingi inapokuwepo haja ya kumwachisha kazi/kuacha kazi/mfanyakazi kila upande utampa taarifa mwenzake kwa utaratibu ufuatao:-

MUDA KAZINI MIAKA:TAARIFA YA KUACHA/ KUACHISHWA KAZI MUDA:MALIPO BAD ALA YA TAARIFA

Miaka 1-3 Miaka 3-6 Zaidi ya miaka 6Mwezi mmoja (1) Miezi miwili (2) Miezi mitatu (3)Mshahara wa mwezi mmoja (1) Mishahara. ya miezi miwili (2) Mish.ah.ara ya miezi mitatu (3)

8.2 Mfanyakazi anapoacha au kuachishwa kazi baada ya kufuata taratibu za hapo juu alipwe haki zake mara moja kama Mkataba huu unavyosema.

8.3 Mfanyakazi anapoacha kwa kufata taratibu kama hapo juu alipwre haki zake mara muda wa taarifa (notice) unapokwisha.

8.4 Mfanyakazi atakayeacha au kuachishwa au kustaafu kuanzia miaka 2 na kuendelea atalipwa gratuity 30% x mishahara ya mwezi (Basic) x 12 x miaka aliyofanya kazi.

9.0 UPUNGUZAJI WA WAFANYAKAZI

9.1 Pande zote mbili zimekubaliana kujizatiti katika kulinda nafasi zao za kazi zilizopo na kufanya kila juhudi kuzuia uwezeka.no wa kupunguza wafanyakazi ambao tayari wana nafasi zao za ajira.

9.2 Upunguzaji wa wafanyakazi utachukua nafasi tu baada ya uongozi wa kutoka Idara moja kwenda nyingine mpaka hapo hali itakapokuwa nzuri au utaratibu utatumika kupunguza wafanyakazi pamoja na zoezi hilo masuala yafuatayo yazingatiwe:

(a) Juhudi

(b) Muda kazini

(c) Masuala ya afya

(d) Uwezo wa kufanya. kazi (Uzoefu)

(e) Umri

(f) Wale wrote wanaopunguzwa kazi wawe wa. kwanza kurejeshwa kazini.

9.3 Imekubalika ya kuwa kwa madhumuni ya Mkataba huu kupunguza wafanyakazi ina maana ya kuwaachisha kazi. bila ya makosa yao wenyewe. Hivyo, muundo wa kuacha/kuachishwa utumike katika malipo wakati wa. kupunguza. aya ya 6.1, 6.2, 6.3 na 6.4 hapo juu.

10.0 MASAA YA ZIADA (OVERTIME)

10.1 Mfanyakazi atakayefanya kazi masaa ya ziada katika siku za kawaida atalipwa mara moja na nusu ya saa atakazokuwa amefanya kazi na siku za Jumapili na sikukuu atalipwa mara mbili ya saa. atakazokuwa amefanya kazi mfanyakazi asipewe (off) badala ya malipo.

11.0 LIKIZO

11.1 LIKIZO YA MWAKA

Katika utumishi wa miezi kumi na miwili (12) mfanyakazi atakuwa na haki ya kupumzika siku 28. Pia mfanyakazi atalipwa nauli kwa ajili ya kwenda likizo yeye na familia yake ikihusishwa na nauli ya wakati huo kwenda na kurudi pamoja na Allowance ya Tshs. 30,000/= (Elfu thelathini tu) Mme/Mke/na watoto wane kwa kila mwaka.

11.2 LIKIZO YA DHARURA

(i) Likizo ya siku saba (7) au zaidi yenye malipo itatolewa kwa mfanyakazi akifiwa na Baba/ Mama/ Mke/ Mme nay a watoto walioandikishwa kisheria na isipunguzwe katika likizo ya mwaka.

(ii) Mkopo wa Tshs. 100,000/= (Laki moja) utatolewa kwa mfanyakazi akifiwa na mmojawapo aliyetajwa hapo juu. Hata kama bado anadaiwa mkopo mwingine, mkopo huo utalipwa. kwa kipindi cha miezi kumi na miwili (12).

(iii) Likizo nyingine nje ya sababu hizo hapo juu itakuwa haina malipo siyo ya mwaka wala kufiwa.

12.0 LIKIZO YA UGONJWA

Mfanyakazi atakayekosekana. kazini kwa rahusa. na idhini ya Daktari anayetambulika, kwa mwajiri na serikali na kuambatana. na vielelezo, kam ED, atahesabika yuko likizo ya ugonjwa.

13.0 MATIBABU

13.1 Pande zote mbili zinakubaliana kwamba wafanyakazi wapewe huduma za matibabu katika zahanati au Hospitali iliyoteuliwa na kiwanda. Ikiwa pamoja na Mke/Mme /na watoto wake walioandikishwa kikampuni wasiozidi watoto wane (4) na mwajiri atapaswa kutoa sick-sheet (hati ya matibabu) kima cha chini matibabu yawe Tshs. 100,000/ =

13.2 Mwajiri atazingatia taratibu za afya na usalama wa wafanyakazi kama ilivyotafsiriwa katika. sheria ya Afya na Usalama. OSHA ACT.

13.3 Ili kupunguza matatizo yanayowakabili wafanyakazi wanaougua na kulazwa Hospitali mwajiri atamlipa mgonjwa anayehusika. Gharama za matibabu kufuatana na taratibu za kiwanda zitatumika.

14.0 VIFO NA MAZISHI

14.1 Gharama za mazishi zitatolewa kwa mfanyakazi aliyefariki akiwa bado katika utumihsi au jamaa ya mfanyakazi akiwa Mke/Me/Baba/Mama au watoto.

14.2 Mwajiri aatoa. sanduku, SANDA, Shada. la maua, fedha aslimu Tshs. 150,000/= zikiwa ni rambirambi kwa wafiwa.

14.3 Endapo mfanyakazi wa Kiwanda cha NBCL Baba/Mama/Mke au mtoto atafariki na iwapo jamaa ya marhemu wTatataka kusafirisha maiti kiwanda kitagharamia usafiri wa. maiti hadi kwao na marehemu au jamaa zake watakapohitaji azikwe, hii ni pamoja na gharama zote za No. 11.1 na 11.2 hapo juu.

14.4 Mwajiri aanzishe mfuko wa Bima kwa ajili ya wafanyakazi.

15.0 SARE ZA KAZI NA VIFAA VYA KUHTFADHIA MWILI

15.1 Kwa wafanyakazi wote wa Idara ya uzalishaji, Ulinzi wahudumu wa Ofisi, Madereva, mafundi n.k. watapewa Jozi mbili, safety boot jozi moja, za sare kila mwaka na vifaa vinginevyo vya kuhifadhi mwili popote wanapohitajika sehemu za kazi.

15.2 Mfanyakazi atakayepewa nguo, safety boot, vifaa vya kuhifadhi mwili atalazimika kuzivaa/kuvitumia katika nyakati zote za kazi.

15.3 Mfanyakazi ambaye atagunduliwa kuwa hatumii nguo zake za kazi au vifaa vya kazi kujikinga ataadhibiwa chini ya sheria ya Afya na kazini. Vinevyo zikiwepo sababu za msingi.

15.4 Mfanyakazi atatakiwa kuleta. vifaa vya zamani kabla hajakabidhi vipya, vinginevyo alipe gharama.

16.0 MKOPO (LOAN)

16.1 Kiwanda kitakuwa kinatenga fedha, kila mwaka kwa ajili ya mikopo kwa wafanyakazi kiasi cha mkopo kitategemea uzito wa shida ya mfanyakazi. Mkopo utakaorahusiwa usizidi mshahara wa miezi sita (6)malipo ya mkopo yatakuwa kwa muda usiozidi miezi kumi na miwili (12).

16.2 Kwa shida ndogondogo (Advance) ziendelee kutolewa kama zinavyotolewa.

17.0 KUSTAAFU/KUSTAAFISHWA

Utaratibu wa kiinua mgongo (gratuity) utumike kwa kila mwezi kama taratibu zilivyowekwa.

17.1 Mtumishi anaweza kustaafu kazi kwa sababu mojawapo ya zifuatazo:

(i) Anafikisha umri wa kustaafu kwa lazima yaani umri wa miaka 60

(ii) Kustaafu kwa hiari baada ya umri kufikia miaka 55

(iii) Kustaafu kwa sababu ya afya mbaya yna Daktari kuthibitisha kwamba afya yake haimruhusu kuendelea na kazi.

17.2 Mwajiri atatoa zawadi ya kumuaga mstaaafu asilimia 80% ya thamani ya zawadi zitakazoamliwa na wafanyakazi watachangia 20%

18.0 MFANYAKAZI BORA/HODARI

18.1 Kila mwaka kila idara itakuwa imechagua mfanyakazi bora na huyo mfanyakazi atapewa kiasi cha Tshs. 200,000/= kuendelea.

19.0 MPANGO WA UFANISI WA KAZI (TIJA)

19.1 Tumekubaliana kwamba ili kuinua ufanisi wa kazi katika kiwanda mambo yafuatayo yanahitajika.

(a) Tujitahidi kutumia vyombo vya kufanyia kazi kwa uangalifu zaidi.

(b) Matumizi bora ya saa za kazi

(c) Uagizaji haraka kwa vipuri vya mitambo kabla ya vingine havij aharibika.

(d) Kutengeneza mitambo kwa ustadi sana mara inapopelekwa katika karakana.

(e) Utii na uaminifu kazini

(f) Matumizi bora ya magari na mitambo iliyopo

(g) Kustawisha njia bora za kuzalisha. mali.

20.0 NIDHAMU KATIKA KAZI

Kila mfanyakazi atatakiwa:

(i) Kutunza siri za kiwanda/Kampuni/Shirika

(ii) Kuwaheshimu viongozi wake

(iii) Kuheshimu kazi yake na kufanya kama anavyoelekezwa

(iv) Kuheshimu wafanyakazi wenzake

(v) Ivuwa mahali pa kazi wakati wote unaotakiwa

(vi) Kuwa msafi kila wakati

(vii) Kutunza usafi wa vyombo vya kazi

(viii) Kuheshimu wageni na wanachama na kuwahudumia vizuri

(ix) Kuipenda kazi yake na kuifanya kwa moyo wote

(x) Kutii kanuni zote za mwajiri na maagizo yanayotolewa na viongozi

21.0 KUPUMZIKA KAZI KWA MUDA (LAY OFF)

Itokeapo au ifikiapo hali ya kusimamisha kazi kwa muda au kutokana na msimu wa uzalishaji kwa muda usiojulikana/kwa. muda utakaojulikana katika kiwanda imekubaliwa kuwa:

(a) Mwajiri kwa haraka atajulisha Tawi la TUICO hali ilivyo

(b) Matayarisho ya haraka ya kukutana kushauriana kuhusu hai hiyo na hatua zitakazochukuliwa kukabili tatizo hilo yatafanywa na mwajiri, kwa kushauriana na Tawi la TUICO kiwandani hapo na TUICO Mkoa.

(c) Wafanyakazi watakapopumzishwa watalipwa nusu mhshara kwa muda wa miezi mitatu na endapo itazidi miezi mine wafanyakazi wataachishwa kazi na kulipwa haki zao wanazostahili.

22.0 VIWANGO NA NGAZI ZA MISHAHARA

Nyongeza za mishahara zitatolewa. kwa wafnayakzi wot na Utawala kwa kushirkiana na Tawi (TUICO) kulingana na utumishi wa muda wa mfanyakazi aliotumikia kazini katika ajira yake na kufuatana na Elimu, uzito wa kazi, Ujuzi, Taaluma ya kazi n.k.

23.0 NYONGEZA YA MISHAHARA

MUDA WA UTUMISHIKIWANGO CHA KUANZIANYONGEZA YA KILA MWAKAMWISHO WA KIWANGO

1. Mwaka 1 hadi 3Tshs. 750,00070%Tshs. 150,000

2. Miaka 3 hadi 6Tshs. 750,00050%Tshs. 225,000

3. Miaka 6 na kuendeleaTshs. 225,00050%Tshs. 339,000 na kuendelea

23.1 Kila mwaka TUICO na management watakaa na kuzungumzia nyongeza ya mishahara.

24.0 NYONGEZA MAALUMU YA MSHAHARA

Mfanyakazi anaweza kuongezwa mshahara maalumu (mara mbili katika kipindi kimoja ikiwa:-

(i) Amekuwa mfanyakazi bora

(ii) Amefuzu mafunzo ambayo yanamruhusu kupata nyongeza hizo kwa mujibu wa mu undo wa utumishi kwiandani unaoruhusu.

(iii) Mfanyakaziatapandihwa cheo kufuatana na juhudi zake kazini na pia atalipwa marupurupu ya uongozikufuatana na cheo chake hicho kipya.

25.0 ADA YA MWANACHAMA

Ada ya mwanachama wa TUICO zitakatwa 2% kutokana na kipato cha mfanyakazi/mwanahama na kiasi hicho kama malipo ya huduma za chama na kuwasilishwa makao makuu ya TUICO kupitia kwa katibu wa Mkoa.

26.0 CHAKULA CHA MCHANA

Utaratibu wa chakula Canteen kwa kampuni uendelee kama ulivyopangwa.

27.0 MPANGO WA UFANISI WA KAZI (TIJA)

Mfanyakazi ataendelea kupewa zawadi ya X-mas kila mwaka ili kusherekea sikukuu hizo.

28.0 POSHO YA SAFARI ZA KIKAZI

Mfanyakazi atastahili malipo ya posho ya safri za kikazi nje ya riba na ndani ya nchi kwa kiwango vilivyowekwa. na serikali.

29.0 SACCOS

29.1 Mwajiri wa TUICO Tawi, lazima wakae pamoja na kuwaelimisha wafanyakazi jinsi ya kuanzisha Saccos. Mwajiri atagharimia mkutano wa saccos na vifaa ikiwa ni pamoja na gharama za mafunzo. Baada ya hapo Saccos itaanzishwa sehemu ya kazi.

30.0 ELIMU NA MAFUNZO

30.1 Kila mfanyakazi atastahili kupewa mafunzo ya juu ya utaalamu wake ndani au nje ya nchi kama ni lazima ili kuongeza ujuzi na utendaji bora wa kazi.

30.2 Mfanyakazi aliyepelekwa mafunzo hataruhusiwa kubadili masomo yake bila idhini ya mwajiri wake.

30.3 Mfanyakazi atakayebadilisha masomo bila idhini ya mwajiri wake atarudishwa nyumbani au atalipa gharama zote za masomo hayo yeye mwenyewe kama gharama hizo hazijalipwa.

31.0 BONUS

Utaratibu wa kulipa Bonus kila siku kufuatana na uzalishaji mali/uendeshaji mali uendelee na pia ulipaji bonus kwa wafanyakazi wote kila mwaka uendelee na itolewe kwa wakati mwafaka.

32.0 MWISHO

32.1 Upande wowote utakaovunja kifungu kimojawapo ndani ya Mkataba huu hatua kali ya kisheria zitumike mara moja.

32.2 Kwa kuwa tunaamini kwamba mali ya Kampuni ndiyo msingi wa Ajira, wafanyakazi tuwe wa kwanza kulinda mali hii na atakayebainika na uharibifu wa aina yoyote hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

33.0 SAHIHI

33.1 Mkataba huu umetiwa sahihi .........

mwezi.....200......

katika Ofisi ya........

Kwa niaba ya

CHAMA CHA WAFANYAKAZI (TUICO)

Kwa niaba

MENEJIMENTI YA.

KATIBU WA TUICO MKOA

MENEJA

MWENYEKITI/TUICO TAWI

TZA Nyanza Bottling Co.Ltd - 2013

Start date: → 2013-01-01
End date: → Not specified
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → 2013-01-01
Name industry: → Manufacturing
Name industry: → Manufacture of beverages
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Name company: →  Nyanza Bottling Co.Ltd
Names trade unions: →  Chama Chawafanyakazi Wa Viwanda, Biashara, Taasisi Za Fedha, Huduma Na Ushauri (TUICO)

SICKNESS AND DISABILITY

Maximum for sickness pay (for 6 months): → Not specified %
Provisions regarding return to work after long-term illness, e.g. cancer treatment: → 
Paid menstruation leave: → No
Pay in case of disability due to work accident: → Yes

HEALTH AND SAFETY AND MEDICAL ASSISTANCE

Medical assistance agreed: → Yes
Medical assistance for relatives agreed: → Yes
Contribution to health insurance agreed: → No
Health insurance for relatives agreed: → No
Health and safety policy agreed: → Yes
Health and safety training agreed: → No
Protective clothing provided: → 
Regular or yearly medical checkup or visits provided by the employer: → No
Monitoring of musculoskeletal solicitation of workstations, professional risks and/or relationship between work and health: → 
Funeral assistance: → Yes

EMPLOYMENT CONTRACTS

Trial period duration: → 90 days
Part-time workers excluded from any provision: → 
Provisions about temporary workers: → 
Apprentices excluded from any provision: → 
Minijobs/student jobs excluded from any provision: → 

WORKING HOURS, SCHEDULES AND HOLIDAYS

Working days per week: → 6.0
Paid annual leave: → 28.0 days
Paid annual leave: → 4.0 weeks
Rest period of at least one day per week agreed: → Yes
Provisions on flexible work arrangements: → 

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Adjustment for rising costs of living: → 0

Extra payment for annual leave

Extra payment for annual leave: → TZS 30000.0

Meal vouchers

Meal vouchers provided: → Yes
Meal allowances provided: → No
Free legal assistance: → 
Loading...